Taasisi kadhaa za dini ya Kikristo zenye mrengo wa kilokole, zinaendelea kusisitiza kuwa, dunia imefika mwisho na kwamba zimebaki siku nne.
Mei 21, 2011 inaelezwa kwamba ndiyo siku ya hukumu (kiyama) na baada ya hapo, dunia itapita miezi mitano kabla ya kuangamizwa kabisa Oktoba 21, 2011.

Taasisi ya American Family Association (AFA) kupitia redio yake ya Family, imekuwa ikieneza ujumbe duniani kote kwamba dunia imefika mwisho.
Mbali na radio hiyo ambayo inasikika ulimwengu mzima, pia AFA imekuwa ikieneza ujumbe huo kwa njia ya vipeperushi ambavyo vilisambazwa duniani kote, ikiwemo Tanzania.
Mbali na taasisi hiyo, pia zipo nyingine ambazo zinashadadia siku hiyo kwa kutoa ushahidi wa maandiko ya Biblia kuwa Mei 21 ni siku ya hukumu.

Mitandao mingi ya intaneti hasa ile inayoendeshwa na madhehebu ya kilokole nchini Marekani, imekuwa ikihubiri kwa nguvu kwamba ni vyema watu wasijisahau kwa sababu dunia imefika ukingoni.
Kwa mujibu wa Family Radio, siku hiyo ya hukumu ndiyo Yesu atarejea na kuwabeba watakatifu wote.
MEI 21 NA WAUMINI WA TANZANIA
Mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein alitoa tamko lake kwa gazeti hili juu ya siku hiyo kuwa hakuna binadamu anayeijua.

Sheikh Yahya alisema: “Watu wanaweza kusema siku fulani ni mwisho wa dunia, lakini hakuna anayeijua. Siri ya siku ya kiyama anayo Mungu peke yake.”
Licha ya kwamba Sheikh Mkuu nchini, Mufti Issa Shaaban Simba hajatoa tamko kwa Waislamu kuhusu siku hiyo lakini waumini wa dini hiyo wamekuwa wakikanusha.
Majid Muhsin, mkazi wa Kariakoo aliliambia gazeti hili kuwa, kwa Waislamu ni kosa kuamini kuwa Mei 21 ni mwisho wa dunia.
“Waislamu tunaamini kuna kiyama lakini haikubaliki kusema siku hiyo ndiyo yenyewe. Hakuna anayejua Kiyama ni lini,” alisema Majid.

Gazeti hili lilitembea kwenye makanisa ya kilokole yanayoongozwa na viongozi wenye majina makubwa nchini ambao nao walidai hawajaelezwa kuhusu mwisho wa dunia.
Daniela Kamau anayeabudu katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) la Askofu Zachary Kakobe alisema kuwa haamini Mei 21 ni mwisho wa dunia.
“Kama kanisa hatujaelezwa kuwa dunia imefika mwisho. Tumeambiwa anayejua siku ya mwisho ni Mungu tu,” alisema Daniela.
Kwa upande wa Highness Paul ambaye ni muumini wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God linaloongozwa na Mchungaji Getrude Rwakatare alisema:

“Siku ikija tutakufa lakini sisi kanisani tumeambiwa hakuna anayejua siku ya mwisho.”
Wakati huo huo, watu mtandaoni wamekuwa wakidai kwamba, inawezekana Mei 21, mwaka huu ni kiyama kwa sababu Marekani wanadai wameshamuua Osama bin Laden.
Kwa upande mwingine, watoa maoni wanadai kwamba, Mei 21 ni namba za kundi la Freemasons kwa hiyo siku hiyo haina uhusiano wowote na Mungu

Kwa Hisani Ya Global Publishers Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)