SPIKA ANNE MAKINDA AFUNGUA SEMINA YA MAJADILIANO NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA VISIVYO NA WABUNGE BUNGENI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SPIKA ANNE MAKINDA AFUNGUA SEMINA YA MAJADILIANO NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA VISIVYO NA WABUNGE BUNGENI


 Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akifungua semina ya majadiliano na viongozi wa vyama vya siasa visivyo na wabunge Bungeni kuhusu uanzishwaji wa chombo cha kupokea maoni ya wananchi juu ya uundwaji wa Katiba Mpya ofisini kwake leo 17/05/2011. Huu ni uratibu mpya ambao Ofisi ya Spika imejiwekea kwa lengo la kukutana na kujadiliana na wadau mbalimbali wa kisiasa, Taasisi za dini, sekta binafsi na vyombo vya habari ili kujenga msingi imara wa mjadala mpana wa uundwaji wa Katiba mpya. Leo Spika Makinda amekutana na wadau kutoka vyama vya siasa vilivyosajiliwa vya UMD, AFP,NLD, UPDP, NRA na APPT-Maendeleo. Kushoto kwa Spika ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria Mhe. Angela Kairuki.
 Mkurugenzi kutoka AFP Bi Nasra Asenga akitoa maoni.
 Wadau wa semina hiyo wakifuatilia ufunguzi kwa makini. Katika Semina hiyo Spika amewataka wadau kuweka uzalendo mbele na kuuenzi umoja wa kitaifa.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Fedha za Serikali Mhe. John Momose Cheyo (katikati) akifafanua jambo kwa ujumbe wa Kamati ya Hesabu za Fedha Serikali kutoka kaitika Bunge la Kenya leo
Mjadala unaendelea.Picha na Prosper Minja-Bunge

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages