SHEREHE ZA UTAMADUNI NA MUUNGANO WA TANZANIA ROMA KUFANYIKA JUMAMOSI HII MEI 21, 2011 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SHEREHE ZA UTAMADUNI NA MUUNGANO WA TANZANIA ROMA KUFANYIKA JUMAMOSI HII MEI 21, 2011



Ndugu marafiki wa Jumuiya ya Watanzania Roma na Watanzania kwa ujumla. Ile sherehe yetu ya Utamaduni wa Tanzania na Muungano wa Tanzania ambayo ilikuwa inasubiriwa na wengi ambayo ilikuwa ifanyike tarehe 30 april 2011 na kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu tukaisogeza mbele, itafanyika jumamosi hii tarehe 21 Mei 2011 kuanzia saa tisa na nusu mchana kwenye ubalozi wa Tanzania Italy, mjini Roma uliopo kwenye mtaa wa Via Cortina d'ampezzo 185. Tunapenda kuwakaribisheni kwa wingi ili muje tujumuike nasi kushereke tukio ili. Kwa wale wote ambao watataka maelezo zaidi mwaweza kuwasiliana na Katibu kupitia e-mail hii ya Jumuiya watanzaniaroma@yahoo.it au kwa simu namba 3479094800. Asanteni na karibuni sana.

Mungu ibariki Africa Mungu Ibariki Tanzania.
wenu,
Andrew Chole Mhella
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages