Ridhiwani akisisitiza jambo kwenye mkutano huo,ambapo aliwapa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa DP,Mchungaji Mtikila siku saba za kunanusha uzushi huo.
Mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kukanusha tuhuma za kumiliki mali zinazodaiwa kuzushwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Demokratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.
Akifafanua jambo kwenye mkutano huo uliofanyika Hoteli ya New Afrika, Dar es Salaam.
Ridhiwani Kikwete akitoka kwenye mkutano. kulia ni Mwandishi wa Habari wa gazeti la Nipashe, Peter Mwendapole
--
...Unaweza kuonekana unaendesha Benzi, kumbe umeliazima, lakini watu wanaokuona wanasema jamaa ana Benzi!". MWANANCHI, Jana Jumanne, Mei 3, 2011.
Ridhiwan alikuwa akiongea na watangazaji wa habari kujibu tuhuma kuwa yeye ni bilionea.Ridhiwani amesema ana shamba bagamoyo la eka moja na nusu. Gari ndogo,Toyota Camry na akaunti CRDB,Stanbic na NBC
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)