BENKI YA KCB - TANZANIA YATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA AMANI ORPHANAGE CENTER - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BENKI YA KCB - TANZANIA YATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA AMANI ORPHANAGE CENTER


 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye akimkabidhi mtoto Beatrice Phinius wa kituo cha watoto yatima Amani Orphanage Centre cha Boko moja ya misaada iliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa ajili ya watoto wa kituo hicho. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa kituo hicho Margaret Mwegalawa.
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye akimkabidhi mtoto Jack Saguno wa kituo cha watoto yatima Amani Orphanage Centre cha Boko moja ya misaada iliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa ajili ya watoto wa kituo hicho. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa kituo hicho Margaret Mwegalawa.
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye (Kushoto) akiteta jambo na Afisa Mahusiano kwa Umma wa benki hiyo Gigi Maajah mara baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi msaada kwa Kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre cha Boko jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye akishirikiana na Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre cha Boko jijini Margaret Mwegalawa kupanga baadhi ya vyakula na vifaa vilivyotolewa kaama msaada na benki hiyo wakati wa hafla iliyofanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko wa Benki ya KCB Tanzania Yusuf Shenyagwa akisaidiana na mfanyakazi mwenzake kushusha mchele uliotolewa na benki hiyo kwa kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.
 Watoto yatima wa kituo cha Amani Orphanage Centre cha Boko jijini wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi msaada uliotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo wenye thamani ya milioni 1.5 kwa watoto 60 wanaolelewa kituoni hapo.
Baadhi ya misaada iliyotolewa na KCB TANZANIA kwa kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre cha Boko jijini Dar es Salaam. Benki hiyo ilikabidhi mchele, sukari, Unga wa Sembe, nguo za aina mbalimbali zikiwemo shuka za kujifunika na kitanda cha mtoto mdogo vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 1.5/-
---
BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kufundishia kwa watoto wanaolelewa na kituo cha Watoto yatima cha Amani Orphanage Centre kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 1.5/- iliyofanyika kwenye kituo hicho kilichopo Boko nje kidogo ya jiji, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye amesema msaada huo umetokana na michango mbalimbali iliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo.
 
Akifafanua Christine amesema kwa kuwa wao ni taasisi ya kifedha wana wajibu wa kurudisha kiasi cha faida kinachopatikana kwa jamii na kwa kuanzia wafanyakazi wa benki hiyo walipendekeza msaada huo uanze kutolewa kwa yatima wanaolelewa na kituo cha Amani Orphanage Centre kutokana na uhitaji walionao.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho Margaret Mwegalawa amesema licha ya benki hiyo kujitolea kukisaidia kituo chake kwa mara ya pili bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ubovu wa jengo na ukubwa wa jukumu la kuwalea watoto 60 wanaolelewa kituoni hapo.
 
Kwa upande wake Beatrice Phinius aliishukuru KCB Tanzania kwa kwa kuguswa na kuwapelekea msaada huo na kuomba taasisi zingine kujitokeza kuiga mfano huo.
 
Mwaka jana benki hiyo licha ya kutoa msaada wa` vifaa mbalimbali wenye thamani ya zaidi milioni 2/- kwa ajili ya takribani watoto 45,  wa shule hiyo kile kinachopatikana, pia ilichukua jukumu la kuwalea watoto 11 wa kituo hicho kwa kuwanunulia vifaa muhimu vya shule.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages