Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein,alishiriki katika mazishi ya Msanii maarufu wa muziki wa Taarab,Maulid Mohamed Machaprala,aliyefariki na kuzikwa jana kijijini Bambi,wilaya ya kati Unguja,pichani Dk Shein,akitia udongo katika kaburi kama isharakatika mazishi hayo.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akishiriki na waumini wengine wa dini ya kiislamu kusalia Jeneza la marehemu Msanii Mzee Maulid Mohammed Machaprala, katika msikiti Nambar,Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.
WANANCHI wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Maulid Machaprala baada ya kusaliwa msikiti Nambari Mwembetanga baada ya sala ya Ijumaa,
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,pichani na waislamu wengine wakishuhudia harakati za mazishi ya Msanii Maarufu wa muziki wa Taarab,Maulid Mohamed Machaprala,aliyezikwa kijijini Bambi wilaya ya kati Unguja leo.
Sehemu ya umati wa waumini waliohudhuria mazishi wakijipanga kwa ajili ya kuliupokea jeneza lililobeba mwili wa Ustaadh Machaprala.Picha zote na Mdau Othman Maulid Othman-Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)