PETER MSIGWA: CCM WANATUMIA RADIO KUNICHAFUA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

PETER MSIGWA: CCM WANATUMIA RADIO KUNICHAFUA


Mbunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mchungaji Peter Msigwa ametoa madai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza kutumia mbinu chafu za kumchafua ambapo amesema kuwa chama hicho kinatumia   moja kati ya Radio zilizopo mkoani mkoani Iringa chini ya mfanyabiashara mmoja ambaye jina la mafanyabiashara  hakulitaja. Pamoja na mbunge Msigwa kuitaja Radio hiyo na watangazaji wake watatu ambao wamekuwa wakifanya hujuma dhidi yake bado amewataka wapiga kura wake kutoamini mbinu hizo chafu za CCM na kudai kuwa kupitia maandamano makubwa yatakayofanyika mjini Iringa atawavua gamba watu hao mbele ya wananchi na kuwa amechoshwa na mbinu hizo chafuza CCM zenye lengo la kumdhoofisha na aonekane si chochote mbele ya wapiga kura wa Iringa mjini.Picha na Habari na Mdau Francis godwin

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages