MBUNGE WA CHADEMA MHESHIMIWA TUNDU LISSU ATUNUKIWA NISHANI YA HESHIMA NCHINI MAREKANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MBUNGE WA CHADEMA MHESHIMIWA TUNDU LISSU ATUNUKIWA NISHANI YA HESHIMA NCHINI MAREKANI


MheshimiwaTundu Lissu
--

Nadhani sitakosea kuwashirikisha habari njema kidogo.jana tarehe 6 Mei 2011, Chuo Kikuu cha Bridgeport
 kilichopo mji wa Bridgeport, Jimbo la Connecticut nchini Marekani kimenitunuku nishani ya 'Mwenza wa Heshima wa Chuo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Bridgeport' (Honorary Fellow of the International College). Citation ya nishani hii inasomeka kwamba 'Mheshimiwa Tundu Antiphas Lissu cheo cha Mwenza wa Heshima wa Chuo cha Kimataifa kwa kutambua utumishi wake uliotukuka katika kuendeleza haki za binadamu,ujenzi wa demokrasia na ulinzi wa mazingira katika Tanzania na Afrika...' Kwa Kiingereza: 'In recognition of his inspired service for the furtherance of human rights,  democratic institutions and the protection of the  environment in Tanzania and in Africa..." Tuzo hii  imekabidhiwa kwangu na Mkuu wa Chuo cha Kimataifa Dr. Thomas  J. Ward na Rais wa Chuo Kikuu cha Bridgeport Dr. Neil Albert  Salonen. Kwa wale wote ambao wanaweza kuwa wanajiuliza kwa nini  sijaonekana Mbeya na Nyanda za Juu Kusini,hii ndio sababu ya utoro wangu.Nitajiunga na makamanda wenzangu kuanzia wiki ijayo.
  
 Wasalaam,
  
 Tundu  Lissu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages