MWANDISHI WA ITV NA RADIO ONE FESTO SIKAGONAMO ATWAA TUZO MBILI KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA MWANDISHI BORA WA MWAKA 2010 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MWANDISHI WA ITV NA RADIO ONE FESTO SIKAGONAMO ATWAA TUZO MBILI KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA MWANDISHI BORA WA MWAKA 2010


MWANDISHI WA ITV na RADIO ONE mkoani Mbeya Festo Sikagonamo ametwaa Tuzo Mbili katika kinyang'anyiro cha mwandishi bora wa mwaka 2010.
Tuzo zilizozolewa naye ni pamoja na habari za maralia na habari za Mazingira ambapo aliwaacha washindani wake 9 katika mchakato huo ulioendeshwa usiku huu katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam.
Festo katika habari ya Maralia aliyoitoa ITV ilihusu matumizi ya vyandarua wilayani Kyela katika kutegea ndege wanaokamata kuku pamoja na kuzungushia bustani za mboga mboga kuzuia kuku wasiharibu mbogo mboga hizo badala ya kujikinga na maralia kama lengo la serikali la ugawaji wa net za mbu.
Picha nyingine ya mazingira ilihusiana  na mradi wa wachina wa kuchimba dhahabu wilayani Chunya ambapo walikuwa na mtambo unaochambua na kuchuja dhahabu ndani kwa ndan huku wakiishi katika hali ya kudhihirisha kuchafua mazingira ya mto ambao waliutumia kusafisha dhahabu hiyo huku vinyesi vyao vikitumbukia mtoni.
wakati wakiendelea na kazi zao hapo wananchi kwa upande mwingine wanautegemea mto huo katika kuhudumia maji kwa makazi na shughuli zingine za kiuchumi, maji ambayo tayari yameshachanganywa na kemikali na uchafu.
HONGERA KADOGOO KWA USHINDI  baba USHINDI hongera kwa USHINDI!!!

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages