Safari ya mwisho ya mwanahabari wa gazeti la Mtanzania mkoa wa Ruvuma Happy Kulanga.
Mazishi ya mwanahabari Happy Kulanga leo
Viongozi wa dini wakitoa dua ya mwisho
Mwanahabari Rashid Msigwa akiwa katika mazishi hayo akichukua kumbukumbu za msiba
Marehemu Happy Kulanga (kushoto ) enzi za uhai wake akipokea cheti chake katika moja kati ya mafunzo ya uandishi wa habari za mazingira (JET)
Mwanahabari Francis Godwin (kushoto) akitoa salama za rambi rambi kutoka Ruvuma Press Club na toka Gazeti la Mtanzania ambalo marehemu alikuwa akilifanyia kazi kama mwandishi mkoa wa Ruvuma
Mdau francis godwin (mwenye shati jeusi )akiwa na ndungu wa mwanahabari Happy Kulanga wakati wa mazishi yaliyofanyika leo katika makaburi ya Mlowa Iringa
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Mwanahabari Kulanga
----
----
Akitoa taarifa ya kifo cha mwanahabari huyo msemaji wa familia Shukuru Lwambati alisema kuwa mwanahabari huyo amefariki jana mjini Makambako wilaya ya Njombe ambako alikuwa akiuguzwa na dadake na kuwa baada ya kuzidiwa alikimbizwa kituo cha afya cha Makambako ambako ndiko mauti ilimkuta.
Msemaji huyo ya familia alisema kuwa Kulanga kabla ya kukutwa na mauti alikuwa akisumbuliwa na homa za mara kwa mara na kutibiwa na kuwa kifo chake kimeacha pengo kubwa katika familia yake .
Marehemu ameacha watoto wawili wote wa kiume .
Katika mazishi hayo wanahabari wametoa salam zao za rambi rambi huku kwa upande wa mwajiri wake gazeti la Mtanzania kupitia mhariri mkuu wameeleza kuguswa na kifo hicho na kuungana na familia katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo huku taratibu nyingine zikifanyika.
Ruvuma Press Club pia imetuma salam zake katika familia hiyo ya Kulanga na kuwa enzi za uhai wake marehemu alifanya kazi kwa kujituma zaidi na wakati wote alikuwa ni mwanahabari ambaye alikuwa akiheshimu maadili ya taaluma hiyo.
Mtandao huu na wanahabari wote nchini tunaungana na falimia yake katika kuomboleza msiba huu mzito kwetu sote .
Mtandao huu na wanahabari wote nchini tunaungana na falimia yake katika kuomboleza msiba huu mzito kwetu sote .
Kifo cha mwanahabari mwenzetu kimeacha pengo kubwa na kuacha simanzi kubwa kwetu na familia na ikumbukwe kuwa sote kwa pamoja tulimpenda sana Happy Kulanga ila Mungu kampenda zaidi yetu hivyo hatuna budi kusema jina lake lihimidiwe milele yote na Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi
AMINA.
AMINA.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)