Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi (MB) akizungumza leo na wasanii wote wa sanaa za muziki wa aina zote wakiwemo wa kizazi kipya, bendi, disko, asili, taaribu n.k. kuhusiana na mikakati ya kukuza na kuinua sanaa hiyo. Katikati ni Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Utamaduni Angela Ngowi. Hapo kesho Mhe.Waziri anatarajia kukutana na kuzungumza na wasanii wa sanaa za filamu, maonyesho, na ufundi.
Lengo kuu la mikutano hii kati wa Mhe. Waziri na wasanii ni kuongelea maendeleo ya fani ya sanaa hapa nchini.
Pichani Juu na Chini Baadhi wa wasanii wa muziki wa aina zote waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
BAADHI YA MASTAA WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA WAKIWA NJE YA OFISI ZA BASATA.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)