Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanafunzi wa Shule ya Msingi Simai iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akikagua jengo la ofisi ya CCM ya Tawi la Majenzi iliyopo Kijiji cha Kusale, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la msingi katika , Shule ya Msingi Simai iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwa kwenye Ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Miikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Simai, iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakiwa katika hafla ya kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, alipofika shuleni hapo leo Mei 17 kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi, wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mikoa ya Kusini na Kaskazini pemba.
Baadhi ya wanachama wa CCM na Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia alipowatembelea akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika mikoa ya Kaskizini na Kusini Pemba, leo Mei 17. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)