KESI YA MAHALU: RAISI MSTAAFU MKAPA AKUNJUA MAKUCHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KESI YA MAHALU: RAISI MSTAAFU MKAPA AKUNJUA MAKUCHA



 Rais mstaafu Benjamin Mkapa
-- 
Na Happiness Katabazi

HATIMAYE utetezi wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, umetua rasmi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam.


Mkapa ambaye ni shahidi wa pili wa kesi hiyo alitoa utetezi huo ambao unaweza kuandika historia mpya katika mwenendo wa kesi nchini, kupitia kiapo chake ambacho kimewasilishwa mahakamani na wakili wa mshtakiwa huyo, Mabere Marando.


Katika moja ya vipengele 13 vya kiapo hicho, pasipo kutaja jina, maelezo ya kiongozi huyo mstaafu yanamgusa Rais Jakaya Kikwete ambaye wakati Mkapa akiwa madarakani alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Hiyo inakuwa ni mara ya kwanza kwa rais mstaafu, kutoa utetezi mahakamani kwa kesi inayomgusa mmoja wa waliokuwa wateule wake wakati akiwa madarakani.


Kesi hiyo Namba 1/2007 ambayo Mahalu anashtakiwa pamoja na Grace Martin inasikilizwa na Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ilivin Mugeta.


Katika kesi hiyo, Mahalu na Martin wanatuhumiwa kwa wizi wa shilingi bilioni tatu katika ununuzi wa jengo la ubalozi mjini Rome.


Katika hati ya kiapo chake cha Machi 31 mwaka huu, ambayo imeandaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Nyaraka (The Registration of Documents Act, Cap. 117 of 2002), Mkapa anaeleza kuwa kila kilichofanywa na Mahalu kilikuwa sahihi na kilikuwa na baraka ya serikali aliyokuwa akiingoza toka mwaka 1995-2005.


Ushahidi huo wa rais Mkapa ambao Tanzania Daima inayo nakala yake, umeorodhesha maelezo yake yaliyoainishwa katika vipengele 13.


Mkapa katika utetezi wake huo anadai kuwa mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo la ubalozi lililoko katika mtaa wa Vialle Cortina d’Ampezzo 185 mjini Rome ulizingatia sera ya serikali ya upatikanaji au ujenzi wa majengo ya kudumu ya ofisi na makazi na kwamba ulizingatia maslahi ya taifa.Kwa Habari hii zaidi 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages