HATIMAYE ‘diva’ katika kiwanda cha filamu Bongo, Irene Uwoya (pichani), alfajiri ya Mei 8, mwaka huu, amejifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Regency iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam, Risasi Mchanganyiko lina full data.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Irene alifikishwa hospitalini hapo huku akiwa ameshikwa na uchungu saa 12 asubuhi na moja kwa moja kupelekwa katika chumba cha upasuaji na kujifungua mtoto wa kiume.
“Irene amefikishwa hospitalini hapa akiwa katika hatua za lala salama baada ya kusikia uchungu na mimba yake ilikuwa inakadiriwa kufikia miezi 10,” chanzo chetu cha habari kilitoboa.
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, Risasi Mchanganyiko lilitia ‘maguu’ katika hospitali hiyo na kukutana na ulinzi mkali uliowekwa na mume wa Irene, Hamad Ndikumana ‘Kataut’.
Kataut alikuwa amekaa mlangoni kuhakikisha kuwa hakuna paparazi anayegusa maeneo hayo na kuingia wodini kwa lengo la ‘kumfotoa’ picha mkewe pamoja na kichanga chake.
Irene, mara kadhaa alikuwa akikwepa kusema kitu kuhusiana na ujauzito wake na alisisitiza kuwa hakuna Paparazi wa Bongo ambaye angeweza kumbaini na kumpiga picha.
Katika kuthibitisha hilo, diva huyo anayetamba katika filamu kadhaa, alikimbilia nchini Cyprus ambako mumewe anacheza soka la kulipwa hadi hivi juzi aliporudi kimya kimya.
Irene alifunga ndoa na Kataut mwaka 2008 katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, aliwahi kutoa kilio cha kusaka mtoto alipohojiwa na Mtangazaji Zamaradi Mketema wa Kipindi cha Take-One kinachorushwa na Runinga ya Clouds.
Gazeti ndugu na hili, Amani la Januari 13, 2011 ndilo lililokuwa la kwanza kuandika kuhusiana na ujauzito wake katika habari iliyosomeka; MIMBA YA UWOYA SIRI NZITO.

KWA MSAADA WA GLOBAL PUBLISHER TANZANIA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)