FIESTA FREESTYLE YAFANA VISIWANI ZANZIBAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

FIESTA FREESTYLE YAFANA VISIWANI ZANZIBAR


 Washiriki wakiangusha mashairi yao mbele ya wakazi wa mji mkongwe waliojitokeza jana jioni ndani ya Ngome Kongwe kwenye shindano la kumsaka mkali wa Serengeti fiesta freestyle 2011 ndani ya Zanzibar.
 Mmoja wa watangazaji mahiri wa Clouds FM Ruben a.k.a Ncha Kali akitoa maelekezo kadhaa kuhusiana na shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta freestyle.
 Pichani ndio waliongia robo fainali jana jioni  ndani ya Ngome Kongwe kwenye msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle,washiriki waliojitokeza walikuwa wapatao 24,na kama uonavyo pichani wamebaki washiriki nane ambapo anatafutwa mkali mmoja tu,mpambano unaendelea jioni hii.
 Pichani anaeongea ni mtangazaji wa Clouds Fm,Fatma Hassan a.k.a Dj Fetty akitoa muongozo kwenye mchakato wa kumtafuta mkali wa Serengeti  fiesta freestyle 2o11 ndani ya Ngome Kongwe jana jioni.
 Mashabiki wakifutilia kwa makini mpambano wa hip hop.
 Baadhi ya wana wa Clouds Tv nao wakifuatilia kwa makini shindano la Serengeti Fiesta freestyle 2011.
 Pichani mbele ni wasahii mahiri wa hip hop amba pia ni majaji wa shindano la Serengeti Freestyle 2011 wakifuatilia kwa makini ,kulia ni Chiku Ketto kutoka kundi la The La Familia pamoja na Bonta kutoka The River Camp Soldier.
 Wakali na mahiri wa kuangusha mangona ndani ya Coconut FM,Boa pamoja na Yoram wakiendeleza kuwarusha washabiki waliofika kwenye mchanyato wa kuwasaka wakali wa Serengeti Fiesta freestyle 2011.
 Washabiki mbalimbali waliojitokeza jana jioni ndani ya Ngome kongwe kwenye msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta freestyle.
 Wakazi wa mji Mkongwe na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi jana jioni  kwenye msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti  Fiesta style 2011.
Baada ya kufanyika mkoani Mbeya na kumpata mkali wa Serengeti fiesta freestyle 2011,na sasa imehamia ndani ya Zanzibar leo kwenye ukumbi wa Ngome Kongwe,ambapo anatafutwa mshindi wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta freestyle 2011 ndani ya zanzibar jana jioni

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages