FFU WA NGOMA AFRICA BAND KUUNGURUMISHA MUZIKI KATI YA MIJI YA BONN NA KOLN 28-MAY-2011 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

FFU WA NGOMA AFRICA BAND KUUNGURUMISHA MUZIKI KATI YA MIJI YA BONN NA KOLN 28-MAY-2011



FFU wa Ngoma Africa Band jukwaani tena! 28-05-2011 
mjini Burg satzvey jirani na BONN, Ujerumani

Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFUyenye maskani yake nchini ujerumani, inatazamiwa kutumbuiza katika maonesho ya  Afrika & Orient  Festival,huko mjini Burg Satzvey jirani na miji ya Bonn na Koln,nchini Ujerumani,siku ya jumamosi 28.Mai.2011 kuanzia saa 1.00 usiku.

Kamanda wa kikosi kazi hiko Ras Makunja wa FFU atakiongoza jukwaani kikosi machachari na
kuhakikisha kuwa gwaride la mziki linamfikia kila mshabiki.. bendi hiyo yenye utajili wa wanamziki wenye vipaji wakiwemo wacharaza magitaa wakali kamavile Chris-B,Said Jazbo Vuai,Maxime buanda..na wengineo,Ngoma Africa band pia maarufu kwa tabia  yao ya kuwadatisha akili na kuwatia kiwewe washabiki.

bendi hiyo imetajwa kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika iliyofanikiwa kuufanya muziki ndio daraja na urimbo
wa kuwanasa mamilioni ya wasahabiki katika kila kona duniani...

Ngoma Africa band ilianzishwa mwaka 1993 pia imetajwa na vianzo vingi vya habari kuwa ni bendi pekee ya kiafrika  hiliyo weza kuimiri vishindo vingi vya washabiki sugu barani ulaya..na kila wanapotumbuiza katika maonyesho ya kimataifa wanakuwa na kazi moja tu... nayo ni kuhakikisha washabiki wanapagawa na kudata akili...

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages