Mgombea ujumbe wa mkutano mkuu wa baraza la vijana wa Chadema Taifa (BAVICHA) Dennis Tesha akiwa na bango linalosomeka kuwa Chadema kama Kikombe cha babu, wakati wakiwa katika harakati za kuandamana leo asubuhi mjini Iringa. Pamoja na Chama hicho kunyimwa kibari cha kufanya maandamano lakini bado kimekaidi na kufanya mkusanyiko wa watu na kuendelea na maandamano jambo ambalo linaashiria uvunjifu wa amani.
mabango mbali mbali yamepamba maandamano ya Chadema ambayo leo asubuhi yalianzia kutoka eneo la Kihesa hadi Mlandege katika manispaa ya Iringa ambako viongozi wa kitaifa wa Chadema wamewahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini .
Gari la Polisi likipita katika mitaa walipokusanyika waandamanaji wa Chama cha Chedema, kwa ajili ya kulinda usalama.
Baadhi ya Wafuasi wa Chadema wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali katika maandamano hayo leo asubuhi.Picha na Francis Godwin, Iringa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)