Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nguruka,mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo aliwaeleza wananchi kutoa ushirikiano kwa wajenzi wa barabara ya lami ya Malagalasi-Nguruka yenye urefu wa Km 48, sambamba na ujenzi wa daraja la kihistoria la Malagalasi lenye urefu wa mita 275. Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nguruka,mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo aliwaeleza wananchi kutoa ushirikiano kwa wajenzi wa barabara ya lami ya Malagalasi-Nguruka yenye urefu wa Km 48, sambamba na ujenzi wa daraja la kihistoria la Malagalasi lenye urefu wa mita 275.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila akipongezwa na Diwani Kata itembula(NCCR-Mageuzi)Shukuru Chiza baada ya kuhutubia mkutano wa kuwashukuru wananchi waliompigia kura wa kata hiyo,Katikati ni Mwenyekiti wa Jimbo Venance Mwaka Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila (kushoto), akipongezwa na mmoja wa akina mama wakazi wa jimbo hilo, ambao watoto wao wamebahatika kusomeshwa na mbunge huyo ambaye ameanzisha mfuko maalum wa kuwasomesha watoto wasiopungua 300 kwa gharama ya milioni 60 ndani ya miaka mitano.Tukio hilo lilitokea baada ya mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wapiga kura kwa ushindi alioupata uliofanyika katika Kata ya Itebula.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila(kushoto)akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Joseph Simbakalila(katikati)walipokua wakipata maelekezo kutoka kwa meneja wa wakala wa Barabara nchini TANROADS Mkoa wa Kigoma Bw Haruna Senkuku kuhusu ujenzi wa barabara ya kwanza ya lami ya Kidahwe-Uvinza yenye urefu wa kilometa 76 inayojengwa na Jimbo la Kigoma Kusini Mkoani Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akimuuliza jambo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (katikati aliyevaa tai) walipokuwa wakikagua ujenzi wa Barabara ya kwanza ya lami ya Kidahwe-Uvinza yenye urefu wa Km 76 inayojengwa Jimbo la Kigoma Kusini,mkoani Kigoma. Viongozi hao wawili walitembelea mradi huo mwishoni mwa wiki.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja wa Wakala wa Barabara wa Serikali (TANROADS), Mkoa wa Kigoma,Haruna Senkuku (wa pili kushoto) pamoja na Katibu wa Mkoa wa Kigoma, Sekulu wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa daraja la kihistoria la Malagalasi lililopo katika Jimbo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Joseph Simbakali(Aliyevaa Suti Nyeusi )pamoja na viongozi wengine wa mkoa huo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila wakiangalia eneo patakapojengwa Daraja Jipya la Mto Malagalasi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)