AUA WAZAZI WAKE KWA KUWAKATAKATA NA MAPANGA MKOANI SINGIDA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AUA WAZAZI WAKE KWA KUWAKATAKATA NA MAPANGA MKOANI SINGIDA

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida Celina Kaluba akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na vifo vya watu wanne waliokufa katika matukio tofauti.Picha na Mdau Nathaniel Limu
---
Na Gasper Andrew.
Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani Singida likiwemo la kijana mmoja kuwakatakata wazazi wake wawili kwa panga na kusababisha vifo vyao.Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida Celina Kaluba amesema katika tukio la kwanza mkulima mkazi wa kijiji cha Ngimu Raymond Erasto (26) amewaua wazazi wake  Erasto Kilakuno (78) na mama yake Frida Dule (57)  kwa kuwakata kata kwa panga.

Amesema mauaji hayo yamefanyika Mei 15 mwaka huu saa 1.45 jioni katika kijiji cha Ngimu tarafa ya Mgori na kwamba chanzo cha mauaji hayo inasadikiwa kuwa muuaji huyo alikuwa amerukwa na akili.Aidha Kamanda Kaluba amesema kuwa muda mfupi kabla kijana huyo hajawaua wazazi wake, alimjeruhi Ester Elihuruma (3) kwa kumkata kwa panga sehemu mbali mbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali.

Amesema tayari wameshamkamata mtuhumiwa Raymond na wanakamilisha mambo machache yaliyobakia ili wampeleke hospitali ya Mirembe Dodoma mjini ili kwenda kuhakikiwa akili yake.
Katika tukio jingine Kamnada huyo amesema kuwa dereva wa pikipiki (bodaboda) Juma Rashidi (32) mkazi wa Itigi wilayani Manyoni ameuawa na abiria aliyekuwa anamsafirisha kwenda kijiji cha Tura mkoani Tabora.

Amesema dereva huyo alikatwa kisogoni na kitu chenye ncha kali na  abiria huyo Geu Njongaji na kudondoka chini kisha kuchinjwa shingo.Kamanda Kaluba amesema mtuhumiwa Geu baada ya kufanikisha mauaji hayo alipora pikipiki hiyo T 962 BNF aina ya Sanlag na kukimbia nayo kuelekea kwao kijiji cha Tura.

Hata hivyo muuaji huyo akiendesha pikipiki hiyo kwa mwendo wa kasi hakufika mbali aligonga shina la mti mkubwa na kuumia vibaya.Kaluba amesema Geu aliamua kurudi Itigi kwa ajili ya kwenda kupata matibabu katika hospitali ya misheni ya St. Gasper na ndipo wananchi waliokuwa wamepata taarifa ya dereva wa bodaboda kuuawa walimvamia na kuanza kumpa kipigo.

Amesema hata hivyo Geu aliweza kukimbilia katika benki ya NMB Itigi kwa lengo la kujisalimisha lakini kundi kubwa la wananchi wenye hasira kali lilimfuatilia na kumtoa nje na kumpiga kwa silaha mbalimbali na kusababisha kifo chake.Kamanda Kaluba amesema wananchi hao wenye hasira kali baada ya kukatazwa kuingia ndani ya benki na askari polisi waliokuwa lindoni, walifanya fujo kubwa na kuharibu milango, madirisha na vioo vya magari.

Kaluba amesema polisi inawashikilia Mohammed Masoud (24) na David Nicodemo (25)kuhusiana na mauaji hayo na kuharibu mali ya benki.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages