ALEXIA ANYAKUA TAJI LA VODACOM MISS DAR CITY CENTER - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ALEXIA ANYAKUA TAJI LA VODACOM MISS DAR CITY CENTER

 Vodacom Miss Dar City Center Alexia William
 Mshindi wa pili wa shindano la Vodacom Miss Dar City Center Salha Israel akijibu swali wakati wa shindano hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Alexia William aliibuka mshindi na kutawazwa kuwa mlimbwende wa kituo hicho.


 Salha Israel ambaye ni mshindi wa pili wa shindano la Vodacom Miss Dar City Center akipita na vazi la ubunifu wakati wa shindano hilo ambapo Alexia William aliibuka mlimbwende wa kanda hiyo. Shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja kutoka kundi la Tip Top Connection akiwaburudisha watazamaji waliohudhuria kwenye shindano la Vodacom Miss Dar City Center lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa akimkabidhi mshindi wa kwanza wa taji la Vodacom Miss Dar City Center Alexia William zawadi ya shilingi Milioni 1/- zilizotolewa na waandaaji wa shindano hilo. Anayeshuhudia ni mke wa Meya Slaa, shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dares salaam.
Mshindi wa kwanza wa taji la Vodacom Miss Dar City Center Alexia William akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa pili Salha Israel (Kushoto) na mshindi wa tatu Jenifer Kalokola mara baada ya kutangazwa washindi. Shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dares salaam.
  Vodacom Miss Dar City Center Alexia William akipunga mkono mara baada ya kutawazwa kuwa mlimbwende wa kanda hiyo. Wengine kutoka kulia kwake ni mshindi wa pili Salha Israel, wa pili kutoka kulia ni mshindi wa tatu Jenifer Kalokola, wa kwanza kutoka kushoto ni mshindi wa nne Maryvine Kenzia na kulia  mshindi wa tano Lilian Paulo, shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dares salaam.
Mkuu wa itifaki wa kamati ya Vodacom Miss Tanzania Albert Makoye, Mtaalam wa Masuala ya Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu na Afisa Udhamini wa kampuni hiyo Ibrahim Kaude wakisoma ujumbe wenye jina la mshindi wa Miss University (UDSM)  Chiaru Masonobo ili walitangaze kwenye shindano la Vodacom Miss Dar City Center lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Saalam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages