Mganga wa Tiba Mdadala Rashid Msigwa
Shuhuda Jaffar Masale akiongea na Waandishi wa Habari
Dawa Yenyewe
--
--
MGANGA wa tiba mbadala aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Msigwa kutoka Kigoma Tanzania amedai kuvumbua dawa aina ya 4A 9 Medicine inayotibu magonjwa sugu ikiwemo ukimwi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliotayarishwa na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA) Mtaa wa Welesi Kikwajuni Mjini Zanzibar Msigwa alisema kwamba dawa zake zimetoa mafanikio makubwa sana kwa wagonjwa kadhaa aliowatibu hadi sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliotayarishwa na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA) Mtaa wa Welesi Kikwajuni Mjini Zanzibar Msigwa alisema kwamba dawa zake zimetoa mafanikio makubwa sana kwa wagonjwa kadhaa aliowatibu hadi sasa.
Alisema dawa yake imenza kutumika zaidi ya mikoa 11 ya Tanzania Bara ikiwemo Kigoma, Arusha Mwanza, Iringa na mikoa mengine lakini pia jijini Dar es Salaam pia ametoa huduma hiyo kwa watu kadhaa.
Mganga huyo alisema alipata nafasi ya kwenda Nchini Muscat Oman na kufanya kazi kubwa sana ya kutoa huduma ambapo mgonjwa mmoja alikuwa akimuona kwa real 20 sawa na dola 50 za marekani ambapo wagonjwa wengi waliotumia daa zake walipona.
Matumizi ya dawa yake vipimo vyake unatumia kichupa kimoja au viwili hadi kupona kabisa hata hivyo alikataa kutaja inatokana na aina gani ya miti lakini alisema hiyo ni siri yake kwa kuwa dawa nyingi hutokana na miti ya majani hasa hizo zinazotumiwa katika hospitali kubwa za kimataifa.
Mganga huyo alisikitishwa na kukosekana ushirikiano kwa taasisi za juu za Afya ikiwemo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na ambapo imeshindwa kutambua dawa hiyo aliyodungua na kutibu.
Alisema hadi sasa ameweza kutibu zaidi ya wagonjwa wapatao 800 hapa Zanzibar katika kipindi kifupia alichokaa amekuwa akipokea wagonjwa wengi sana na wa maradhi mbali mbali ikiwemo maradhi ya kisukari, ukimwi na magonjwa ya akina mama.
Akitaja matumizi ya dawa zake Mganga huyo alisema kazi ya dawa hiyo ni kusukuma damu mwilini, kuongeza madini ya chuma, kuongeza kinga katika mwili na kujikinga na maradhi mbali mbali.
Mganga huyo alisema ujuzi wa matumizi ya dawa ambayo imegunduliwa miaka mingi lakini kwa zaidi ya miaka 13 sasa inafanya kazi ya kuwatibu wagonjwa mbali mbali ndani na nje ya nchi hiyo amesema awali dawa hiyo iligunduliwa na mama yake mzazi ambaye ameshafariki muda mrefu lakini kwa zaidi ya miaka kumi na tatu dawa hiyo amekuwa akiitumia kuwatibia watu mbali mbali ndani na nje ya nchi ikiwemo nchini Muscat Oman.
Aidha aliilaumu serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya kwa kushindwa kuitambua dawa hiyo ambayo imeshatibu watu tofauti na imekuwa ikiwapa nafuu wagonjwa wengi wa maradhi mbali mbali kwa madai kwamba dawa yake wanaifanyia utafiti jambo ambalo alisema limekuwa likisuasua.
“Tatizo liliyopo ni kati ya wataalamu wakizungu na sisi waganga wa tiba asili waganga wa dawa hizi za mitishama na ndio maana wakaweka kikwazo hiki kwamba wanaifanyia utafiti jambo ambalo linachelewesha dhana nzima ya utoaji tiba kwa wagonjwa” alisema mganga huyo.
Katika mkutano huo ambayo uliwashirikisha watu wenye kuishi na virusi vya ukimwi na asasi zisizokuwa na kiserikali Mganga huyo alisema dawa yake imetambuliwa na Baraza la Tiba Asilia la Zanzibar pamoja na bodi ya chakula na vipodozi na kwa sasa amekuwa akitoa dawa zake kwa urahisi na wagonjwa wengi wamekuwa wakienda kuchukua dawa zake.
Alisema watu walioathirika na virusi vya ukimwi na wagonjwa wengine wamekuwa wakitegemea dawa zake lakini aliwataka wagonjwa kutovunjika moyo na matumizi ya dawa hizo ambazo amesema yupo tayari kutoa tiba kwa kuwasaidia wagonjwa wanne ambao atawapa dawa bure iwapo watakubali kwenda kuangaliwa afya zao kwanza kabla ya kutumia dawa hizo.
“Mimi sharti langu ni kwamba kabla hujatumia dawa zangu basi hutaka lazima ukachekiwe afya yako na upimwe kwanza ili ukija kutumia nijua ni virusi vingapi ulivyonavyo mwilini na baada ya kumaliza kutumia dozi yangu pia hutaka wende ukapime vile vile ili tujue waliobaki na kama wameshamalizika” alisisitiza mganga huyo.
Akifafanua kwamba baadhi ya watu wenye virusi vya ukimwi kwa watu wenye CD4 kiwango cha 427 na baada ya wiki mbili mgonjwa huyo huyo CD4 zake ziliongezeka na kufikia 613.
“Mimi dawa yangu inayo uwezo wa kuongeza CD4 kwa muda wa wiki moja tofauti na zile za kupunguza makali ya virusi za ARV na kabla ya kumpa mgonjwa dawa nataka kwanza akapime na aje na vipimo vyake ndipo aweze kutumia daa hizi” alisema Msigwa.
Akitoa ushuhuda wa magonjwa yaliokuwa yakimsumbua mmoja ya wagonjwa aliyejitambulisha kwa jina la Jaffar Masale ambaye alidai awali kuwa na ukimwi lakini baada ya kutumia dawa hiyo amepona kabisa kwa mujibu wa vipimo alivyopewa huko katika hospitali mbali mbali alizokwenda kupimwa.
“Kwa kweli niseme kwamba nilikuwa katika hali mbaya sana baada ya vipimo kubaini kwamba nimeathirika na ukimwi na nilikuwa naharisha na ngozi yangu yote kuharibika lakini baada ya kutumia dawa hiyo sasa nipo salama na ninaweza kufanya kazi zangu vizuri sana na ninashukuru kwamba hivi sasa nimepata nguvu ya kufanya kazi” alisema Masale.
Shuhuda mwengine ni mhadhiri wa chuo kikuu, Abdulkadir Mohammed amesema yeye alikuwa akizumbuliwa na malaria sugu ambayo kwa miezi kadhaa amekuwa akitumia dawa bila ya mafanikio lakini baada ya kutumia dawa za Mganga huyo amepona na amekwenda kupima ameonekana amepona kabisa.
“Nilikuwa nimeshachoka kutumia madawa ya kila aina lakini nashukuru kwamba nilipotumia dawa za Dk Msigwa nimepona kabisa lakini nilipokwenda hospitali kupima nikaulizwa nimetumia dawa gani lakini sikutaka kusema dawa niliotumia lakini kwa ufupi dawa nilizotumia ni hizi hizi” alisema mhadhiri huyo katika mkutano huo.
Msigwa alitoa ombi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupatikana kwa mashine ya kujuwa kiwango cha virusi katika damu ya binaadamu inayojulikanana kwa jina la 'Viral load' ili wananchi wapate kwenda kupima afya zao kupitia kipimo hicho.
“Mashine hii ni muhimu sana ambayo ikipatikana itawasaidia wagonjwa kujuwa kiwango cha virusi katika damu yao ....kwa sasa wagonjwa hao wanakwenda Dar-es-Salaam kupima lakini ikipatikana hapa itakuwa rahisi kujulikana vipimo vyao badala ya kupoteza nauli kufuata huduma hiyo mbali”alisema Msigwa.
Msingwa alisema hakuna kipimo hata kimoja kinachoweza kukuonesha mgonjwa ambaye ana vizuri vya ukimwi na baadaa ya kutumia dawa vipimo vikaonesha kwamba hana ukimwi.
“Mimi nawashangaa watalaamu wa tiba unapokwenda kupima daktari anaokwambia kuwa wewe una virusi idadi kadhaa maana idadi ya virusi ni kubwa inafika millioni 50 na zaidi lakini ukishatumia dawa ukenda tenda wanakwambia virusi vyao vimemalizika mwilini sasa kama virusi vimemalizika madaktari wanasita nini kusema kwamba wewe umepona? Alihoji Mganga huyo na kuongeza kwamba “hakuna kipimo duniani kitakachokuonesha kwamba wewe ni positive na baadae upime tena kipimo hicho kiseme wewe ni negative kipimo hicho hakuna duniani kote” alisema.
*Habari hiii na Mdau Salma Said, Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)