Mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Jina Halikuweza Kufahamika Mara Moja Amenusurika Kufa Mara baada ya Kukutwa Alfajili Kwenye Block Ambalo sio lake na Kukisiwa kuwa ni Mwizi Mara baada ya Mwanafunzi Mmoja Kuibiwa Asubuhi Ya Leo.Mwanafunzi Huyo Alikutwa akizubaazubaa Kwenye Block ambalo Sio lake na Halipoulizwa Halikua akitoa Maelezo Ambayo Hayajanyooka Kupelekea Baadhi ya Wanafunzi Kuendelea Kumshushia Kipigo Mwanafunzi Huyo hadi kuumia Vibaya Kichwani.
Mtuhumiwa Huyo Akijielezea Mara Baada Ya Wanafunzi Kusitisha Kumshushia Kipigo Wakati alipokua akihojiwa na Wanafunzi Hao.
Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii Na Sanaa ya Lugha Kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma Mh Leornad Singo (mwenye jezi ya Arsenal) Akizuia Wanafunzi Kutompiga Kijana Huyo ambaye inasemekana si mwanafunzi Wa Chuo Hapo Wakati Yeye Mwenyewe Akisema Kuwa Ni Mwanafunzi Wa Mwaka wa Kwanza wa Chuo Kikuu Cha Dodoma anayesoma Elimu ya Utawala wa Biashara (Business Administration).Huku Wanafunzi Wakidai kuwa Yeye Sio Mwanafunzi Bali Ni Mwizi Na Inasemekana Kuwa Kuna Chumba Ambacho Kinamdhamini Kijana Huyo Kufanya Shughuli za Wizi Hapa Chuo.
Wanafunzi Wa Udom Wakiwa Wamemzunguka Kijana huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika Mara Moja huku wengine wakimhoji na wengine wakiendelea Kumshushia Kipigo Kijana Huyo.
Mmoja Wa Wanafunzi Ambao anaishi kwenye chumba kilichotajwa na Mtuhumiwa huyo Akitoa Maelezo kuhusu Kijana Huyo kama Kweli Ni Mwanafunzi Au Sio Mara Baada ya Mtuhumiwa huyo kuulizwa alifikia Chumbani gani na alilala wapi Na Ndipo wanafunzi Walipochukua Jukumu la Kuwatafuta Wanachumba Waliotajwa na Kijana Huyo ili kutoa Maelezo ya Kutosha kama Kweli wanamfahamu au laaah.
Kama Unavyojua tena Matukio Kama Haya Mashahidi Wa Yehova Huwa Hawakosi kushuhudia ili kupata cha Kuhadithia. Hapa Ni Baadhi ya Wanafunzi Wakishuhudia Tukio Hilo ambalo limepelekea mtuhumiwa huyo Kuumia vibaya pande za usoni na kichwani baada ya kupokea kichapo kitakatifu kutoka kwa wanafunzi wa Udom Ambao Wanahasira ya Kuibiwa Kila Mara.
Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii na Sanaa Ya lugha Mh Singo Akijaribu kumtoa Mtuhumiwa huyo Kwenye Mikono ya Wanafunzi Wenye Hasira ili kumpeleka Kwenye Vyombo Vya Sheria.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)