WANAFUNZI MKOANI MOROGORO WAKIWA TAYARI KWA PASAKA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WANAFUNZI MKOANI MOROGORO WAKIWA TAYARI KWA PASAKA


Wanafunzi wa shule ya misheni ya Agfa James

NA DUNSTAN SHEKIDELE,GPL,MOROGORO
MAANDALIZI ya Sikuu Kuu ya Pasaka yameanza kupamba moto ambapo leo asubuhi mtandao huu ulushuhudia lundo la wanafunzi wa shule ya misheni ya Agfa James iliyopo maeneo ya Nane Nane mkoani hapa wakiangwa na Mkurugenzi wa shule hiyo, Father Rikado Maria, aliyekuwa akitumia usafiri wake wa baiskeli.

Padri huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Radio Ukweli inayomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la Morogoro,amekuwa akiwashangaza baadhi ya watu kutokana na imani yake ya tutovaa viatu na kutembelea usafiri wa baiskeli huku akiwa anamiliki shule mbili za sekondari moja ikiwa maeneo la Area Five.

Mwandishi wetu alipotaka kuzungumza na Padri huyo raia wa ltalia, alidai kwamba ana haraka hivyo asingeweza kuzunguma "Kuna watu nimeahidiana nao tukutane mida hii, hivyo unaweza kunitafuta siku nyingine," alisema Padri huyo.

Baadhi ya wananfunzi waliohojiwa na mwandishi wetu walidai kwamba mkuu wao huyo wa shule ana kawadia ya kutotaka kujikweza kwa misaada anayoitoa katika jamii.

"Tunamshukuru sana Father Rikado kwa moyo wake wa huruma kwani katika shule zake ukidhibitika kwamba wewe ni yatima unasoma bure kidato cha kwanza mpaka cha sita pia habagui waislamu na wakristo, wote tunasoma katika shule yake, jana tulifunga shule kwa mapunziko mafupi ya Sikukuu ya Pasaka," alisema dent Abeli Maiko.



Father Rikado

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages