VITUKO NDANI YA DALADALA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

VITUKO NDANI YA DALADALA

 
NA DUNSTAN SHEKIDELE,GPL,MOROGORO
TIMBWILI kubwa liliibuka  jana ndani ya daladala yenye namba za usajili T226 AEG inayofanya safari zake pande za mjini kueleka Nane nane,kufuatia mtoto mmoja kutaka kutwangana makonde na kondakta chanzo kikiwa ni tangazo lililoandikwa kwenye mlango wa basi hilo.

Mwandishi wetu aliyekuwepo ndani ya daladala hiyo alishuhudia mwanzo mwisho wa ugomvi huo huku baadhi ya abiria wakimuunga mkono mtoto huyo na wengine wakiwa upande wa kondakta.

Ugomvi huo ulianza pale kondakta alipoanza mchakato wa kukusanya nauli kwani  alipofika kwa  kijana huyo  aliyekuwa ameketi kwenye kiti alilipa nauli ya shilingi 150 aliyoisoma kwenye tangazo. Alipotakiwa kutoa kitambulisho cha shule kijana huyo alidai kwamba amemaliza darasa la saba mwaka jana.

"Sina kitambulisho na kwamba mimi sijafikisha umri wa utu uzima nina miaka 15 na kwamba kwenye tangazo lako hapo mlangoni umeandika wakubwa 300 wanafunzi 150, watoto hujaandika sasa naomba maelekezo," alijitetea mtoto huyo.

 
Konda huyo alikataa utetezi huo na kuhoji; "Kama wewe una nauli nusu kwanini toka upande umekalia kiti huku watu wazima wakiwa wamesimama, hapa utalipa nauli kamili hizi kazi ni za watu siyo zetu tafadhali usiniletee usharobaro kwenye kazi," kondakta aling’aka.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya huku kila upande ukitetea msimamo wake,mzee mmoj alimlipia nauli mtoto huyo na ugomvi ukaisha huku baadhi ya watu wakitaka maandishi  yanayoelezea gharama za nauli  yatolewe ufafanuzi ili kuondoa utata kama uliojitokeza.

Hivi karibuni  SUMATRA waliagiza daladala zote kuandika nauli kwenye mlango kwa lengo la kutoa lawama za watu kuongezewa nauli kienyeji.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages