TAMASHA LA ZINDUKA KISESA LAFANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAMASHA LA ZINDUKA KISESA LAFANA

Jana jioni kijiji cha Kisesa wilaya ya Magu, mkoa wa Mwanza kulikuwa na show safi yamtakato ya muziki wa kizazi kipya iliyofanyika kuhamasisha utumiaji wa vyandarua na vita dhidi ya maralia. ZINDUKA.

Fid Q. alikuwa ndiye rais wa mpango huo nae alishiriki vilivyo kutoa elimu sambamba na kutoa burudani kwa hadhira. Duh hadi watoto wanazikwachu songi zake!!  

"Kulala kwenye chandarua hiki kila siku kutakukinga dhidi ya maambukizi ya malaria" Fid Q akimsaidia kutundika mama wa kaya hii mwalimu Pendo Musa wa shule ya msingi Gedeli B.

Kabla ya burudani hiyo . Balozi wa malaria Fid Q alitembelea nyumba kwa nyumba kukagua, kuangalia na kuona kama kaya jeh! zimepata vyandarua? jeh! vinatundikwa? na vinatundikwaje?

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages