Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka DRC-Kongo Faraja Ntaboba akizikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa nyimbo za injili jioni ya leo,kwenye tamasha hilo lililofanyika katika uwanja wa ccm kirumba,jijini Mwanza na kuhudhuriwa na watu kibao. Mmoja wa wakali wa nyimbo za injili nchini,Rose Muhando akiimba wimbo moja ya wimbo wake uliowahi kutamba siku kadhaa za nyuma uitwao nibebe,wimbo huo uliwavutia wengi uwanjani hapo na kujikuta wakicheza na kuimba kwa pamoja,hali iliyomfanya Rose Muhando apandishe mzuka wa kuimba na kucheza zaidi. Mwimbaji nyota wa muziki wa nyimbo za injili,Anastazia Mukabwa ambae kwa sasa anatamba na wimbo wake wa kiatu kivue alioshirikiana na Rose Muhando,akiimba jukwaani jioni ya leo kwenye uwanja wa ccm-kirumba,ambapo ilikuwa ni muendelezo wa tamasha la pasaka lililoanzia jijin Dar,kisha Dodoma na kumalizikia jijini Mwanza,ambapo ilikuwa ni siku ya sherehe za muungano kati ya Tanganika na Zanzibar.
Christina Shusho akiimba jukwaani jioni ya leo mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi kutoka sehemu mbalimbali,ambapo leo ilikuwa ni siku ya Muungano,lakini limefanyika tamasha la muziki wa injili,lililoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions kwa ajili ya wakazi wa jiji la Mwanza ambapo wakazi wake bado walikuwa mapumzikoni.
Anaitwa Bonny Mwaitege ambaye kwa sasa anatamba na nyimbo zake kadhaa ikiwemo ule wa Mama ni Mama pamoja na Njoo ufanyiwe maombi,nyimbo ambazo pia jioni ya leo ameziimba mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza. Nyota mwingine wa nyimbo za injili kutoka nchini DRC-Congo,Solomoni Mukubwa akiwaimbia wakazi wa jiji la Mwanza jioni ya leo kwenye tamasha la nyimbo za muziki wa injili lililowakutanisha wakazi mbalimbali jioni ya leo,ambapo ilikuwa ilikuwa ni siku ya Muungano. Wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia kwa nguvu huku baadhi yao mikono yao ikipunga hewani,jioni ya leo kwenye tamasha la muziki wa nyimbo za injili lililoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions,ya jijini Dar Es Salaam. Baadhi ya nyota wa muziki wa injili,kutoka kushoto ni Rose Muhando,Christina Shusho pamoja na Solomon Mukubwa wakijadiliana jambo kabla ya kupanda jukwaani jioni ya leo kwenye uwanja wa ccm-kirumba,jijini Mwanza. Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama (waandaaji wa tamasha) akimsikiliza kwa makini mmoja wa watangazaji mahiri wa Clouds FM (kituo cha Mwanza),Albert Sengo kuhusiana na albamu mpya ya Anastazia Mukabwa aliomshirikisha Rose Muhando,iitwayo Kivue kiatu,pichani kati ni mfanyakazi wa Clouds FM ndani ya jiji la Mwanza aitwaye Samadu akisikiliza pia
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)