BABU WA LOLIONDO AFIWA NA MWANAE WA KIUME - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BABU WA LOLIONDO AFIWA NA MWANAE WA KIUME


Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ngorongoro, wakiwa nyumbani kwa mchungaji Ambilikile Mwasapila (kushoto), wakimpa pole kutokana na kifo cha Jackson Mwasapila(43), kilichotokea katika hopitali ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara jana. Picha na Mdau Mussa Juma
---
MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu huko Samunge, Loliondo amefiwa na mtoto wake wa kiume jana. Kutokana na msiba huo, Serikali imesitisha tena tiba anayotoa hadi Ijumaa. Habari zilizopatikana kijijini hapo jana zimeeleza kuwa mtoto huyo, Jackson Mwasapila (43), alifariki dunia jana asubuhi, nyumbani kwake wilayani Babati, Mkoa wa Manyara. 

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali aliliambia gazeti hili jana kuwa kutokana na msiba huo, Mchungaji Mwasapila atasitisha tiba kuanzia leo jioni.Mkuu huyo wa Wilaya alifika Samunge jana hiyo hiyo akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, kumpa pole mchungaji huyo. "Tunapenda kutangaza rasmi kuwa huduma zitasitishwa hadi Ijumaa na tunaomba watu walio mbali wasije hadi Ijumaa," alisema Lali.Alisema Serikali itashiriki msiba huo na inajiandaa kutoa msaada wa kumpeleka Mchungaji Mwasapila, Babati kushiriki msiba huo.   

Akizungumzia Juu ya kifo cha Mwanae Mchungaji Mwasapila alisema mtoto wake huyo alifariki jana saa 5:00 asubuhi katika Hospitali ya Wilaya ya Babati baada ya kuugua malaria ghafla. "Taarifa ambazo nimezipata ni kuwa Jackson alikuwa anasumbuliwa na kichwa na baada ya kufikishwa hospitali, alifariki dunia," alisema Mchungaji Mwasapila.

Mchungaji huyo, alisema Jackson ni mtoto wake wa tatu kati ya sita alionao. Wagonjwa wampa poleBaadhi ya wagonjwa waliokwenda Samunge jana kupata tiba, walitoa salamu za rambirambi kwa Mchungaji Mwasapila kutokana na msiba huo.Hata hivyo, wakati wagonjwa hao wakimpa pole, mchungaji huyo alikuwa akiendelea kuwapa dawa kama kawaida.  

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages