SINGULUMA AJIPANGA KUTUA CHELSEA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SINGULUMA AJIPANGA KUTUA CHELSEA

 
Na Khadija Mngwai
MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe, Given Singuluma (pichani) amesema atahakikisha anajituma zaidi uwanjani ili kutimiza ndoto zake za kucheza soka la kulipwa nje ya Afrika hasa katika Klabu ya Chelsea ya England.

Katika mahojiano maalum na Championi Jumatano, Singuluma ambaye ni mfungaji wa bao la kwanza la Mazembe katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Simba wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, alisema, kwa uwezo wake wa sasa anaamini ndoto yake itatimia hivi karibuni.

Singuluma,24, raia wa Zambia, aliliambia gazeti hili kwamba anahitaji kucheza nje ya Afrika ili kudhihirisha kiwango chake ambacho anaamini kinapanda kila siku kutokana na uwezo wake wa kuzisumbua safu za ulinzi za timu pinzani.

“Moja ya mikakati niliyojiwekea ni kuhakikisha nafika mbali zaidi katika kazi yangu ambayo ni mpira wa miguu, nataka kucheza Ulaya, lakini zaidi ni kucheza Chelsea,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Zanaco ya Zambia.

Akizungumzia ushindi wa mabao 3-2 iliyopata timu yake dhidi ya Simba, Singuruma alisema: “Nashukuru kwa ushindi, Simba ni timu nzuri na kuna wachezaji wazuri ambao wanajituma, wanapaswa kujituma zaidi ili wafike mbali.”

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages