MZUNGU WA YANGA ATUA AZAM KWA KISHINDO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MZUNGU WA YANGA ATUA AZAM KWA KISHINDO

 

Na Elius Kambili
KIPA wa Yanga wa zamani, Obren Cuckovic (pichani) amesajiliwa na Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili, imefahamika.

Cuckovic raia wa Serbia aliyeichezea Yanga kwa mafanikio misimu wa 2009/10 na kufanikiwa kuipa ubingwa, alitua nchini wikiendi iliyopita na juzi Jumatatu alisaini mkataba huo.

Kwa mujibu wa habari kutoka Azam, Cuckovic amesajiliwa ili kuongeza nguvu katika nafasi ya ulinzi na kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri msimu ujao wa Ligi Kuu ya Bara.

“Tayari Obren amesaini mkataba wa miaka miwili kucheza katika timu yetu baada ya majadiliano na kufikia muafaka ndani ya muda mfupi, kwa sasa yupo hotelini na anaweza kuanza mazoezi na wenzake muda wowote kuanzia sasa,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa mbali ya kumsajili Obren, wapo katika mipango mikali ya kumnasa mshambuliaji raia wa Benin ambaye atasaidiana na John Boko katika safu ya ushambuliaji.

Azam ambayo jana ilicheza mchezo wa Ligi Kuu ya Bara dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Uhuru, ipo katika vita ya kuwania nafasi pili katika ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages