Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa tamasha la nyimbo za injili lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lililojumisha wasanii wa nyimbo za injili kutoka ndani na nje ya nchi liliratibiwa na kampuni ya Msama production ya jijini Dar es Salaam. Mtoto ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akimsalimia Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baadaya kuwasili katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika tamasha la wasanii wa nyimbo za dini lililofanyika jana.
MBUNGE wa Rombo kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Selasini akimsalimia Rais Jakaya Kikwete kwa furaha ya aina yake, wakati alipokutana na Rais, kwenye Tamasha la wasanii wa nyimbo za injili lililofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akizindua album ya Haleluya collection yenye nyimbo za wasanii mbalimbali wa injili wakati wa tamasha la wasanii wa nyimbo za dini lililofanyika katik ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salam jana mchana.Katikati ni mratibu wa Tamsha hilo Bwana Alex Msama na kulia ni Askofu Samson Kameta.Picha na Freddy Maro-IKULU
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)