MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA AJIUNGA NA CCM MJINI DODOMA JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA AJIUNGA NA CCM MJINI DODOMA JANA


 Mweyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya Bwana Shamwee Shitamabala muda mfupi baada ya kupokea kadi ya CCM mjini Dodoma jana mchana.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM Bwana Sambwee Mwalyego Shitambala aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha CCM baada ya kukihama rasmi CHADEMA katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma jana mchana.
Aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya Bwana Shambwee Shitambala na aliyekuwa katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Ileje Bwana Henry Raphael Kayuni wakila kiapo muda mfupi baada ya kupokea kadi za CCM katika viwanja vya makao makuu ya CCM mjini Dodoma jana mchana
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua mikono ya viongozi waandamizi wa CHADEMA mkoa wa Mbeya waliokihama rasmi chama hicho na kujiunga na CCM mjini Dodoma jana mchana.Kushoto ni aliyekuwa katibu mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Ileje Bwana Henry Raphael Kayuni na kulia ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya Bwana Shambwee Shitambala.kulia ni Waziri wa Maji pia ni mjumbe wa NEC ,CCM Mkoa wa Mbeya profesa Mark Mwandosya.Picha na Freddy Maro-IKULU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages