MAPACHA WA TATU WAPELEKA TUZO ZAO BUNGENI MJINI DODOMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAPACHA WA TATU WAPELEKA TUZO ZAO BUNGENI MJINI DODOMA

Mwimbaji na rapa mahiri wa bendi mpya ya Mapacha Wa3, Khalid Chokoraa (kushoto) akiwa na Meneja wake Dakota Hamis, wakiwa na tuzo yao moja kati ya mbili walizopata katika Tuzo za Tanzania Kili Music Awards hivi karibuni. Hapa wakiwa kwenye Kituo cha Mabasi Ubungo wakati wakiwasubiri wenzao kuwasili kituoni hapo tayari kwa ajili ya kuelekea Bungeni mjini Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha kwa Waheshimiwa Wabunge na kutambulisha ujio wa bendi yao katika jukwaa la Muziki wa Dansi. Chokoraa na wenzake wameondoka leo asubuhi kuelekea mjengoni. Big Up Mapacha Wa3.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages