MKUTANO WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAANZA LEO MJINI DODOMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKUTANO WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAANZA LEO MJINI DODOMA




 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiingia ndani ya ukumbi wa Bunge kuongoza kikao cha kwanza cha mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi  kwa wabunge kuhusu kanuni za uendeshaji wa shughuli za bunge leo mjini Dodoma.
 Wabunge wakiwa katika kipindi cha maswali na majibu ndani ya mkutano wa wa tatu wa kikao cha kwanza cha bunge leo mjini Dodoma
 Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akijibu maswali kutoka kwa wabunge  juu ya ufanyaji wa tathmini na ulipaji  wa fidia kwa wananchi kutoka kwa makampuni yanayofanya utafiti wa madini ya dhahabu nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Sheria na Katiba Celina Kombani akitoa ufafanuzi kwa wabunge kuhusu namna ya kuingia katika zoezi la upatikanaji wa katiba mpya na namna wananchi watakavyoshiriki kutoa maoni yao katika mchakato wa upatikanaji wa katiba hiyo bungeni mjini Dodoma.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mizengo Pinda (kulia)akijadili jambo na Waziri Ofisi ya Rais ,Utawala Bora Mathias Chikawe ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages