MAKAMANDA WA POLISI WILAYA WAPIGWA MSASA WA NGUVU MJINI DODOMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMANDA WA POLISI WILAYA WAPIGWA MSASA WA NGUVU MJINI DODOMA

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, James Nsekela akitoa hotuba ya ufunguzi wa programu ya mafunzo ya wakuu wa polisi wa wilaya nchini katika kubaini, kuzuia na kudhibiti uhalifu kupitia mfumo wa ulinzi shirikishi. Semina hiyo ya siku tatu imefunguliwa jana mjini Dodoma.Kushoto ni Kamanda Mkuu Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Zelote Stephen na Kulia ni Kamanda Mkuu wa Polisi Jamii Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Basilio Matei.
 Mratibu wa Polisi Jamii, Mrakibu mwandamizi wa Polisi, Englibert Kiondo akielezea kuhusu waraka wa Mkuu wa Jeshi la Polisi wakati wa mafunzo ya wakuu wa polisi wa wilaya nchini katika kubaini, kuzuia na kudhibiti uhalifu kupitia mfumo wa ulinzi shirikishi. Semina hiyo ya siku tatu imefunguliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dododoma mjini Dodoma.
 Baadhi ya wakuu wa polisi wa wilaya nchini wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,James Nsekela wakati wa ufunguzi wa programu ya mafunzo ya wakuu wa polisi wa wilaya nchini katika kubaini, kuzuia na kudhibiti uhalifu kupitia mfumo wa ulinzi shirikishi. Semina hiyo ya siku tatu imefunguliwa jana mjini Dodoma. Picha na Hassan  Mndeme-Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages