KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO

 Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku (kushoto) akizungumza jambo na Mbunge wa Igunga Bw. Rostam Aziz (Kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akijibu maswali ya wabunge yaliyoulizwa kuhusu vyombo  vya studio vya kurekodia walivyopewa wasanii na Rais Jakaya Kikwete ili  kupunguza matatizo wanayoyapata katika kazi zao ambapo amesema utaratibu wa ufungaji wa studio hiyo unafanyika ili kutoa fursa kwa wasanii wengi kunufaika kwa gharama nafuu.
 Baadhi ya maofisa wa JWTZ na watendaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa wakitoa salam kwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kutambua uwepo wao ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Naibu waziri wa Ujenzi Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)akifurahia jambo na  Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Alli Iddi (katikati) na Mh.Zakia Meghji (Mbunge wa viti maalum,CCM) nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.
 Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge leo mjini Dodoma kufuatia vurugu zilizotokea jana wakati wa zoezi la ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu uundwaji wa katiba mpya ambapo ametoa wito kwa serikali kuongeza muda zaidi wa ukusanyaji wa maoni na idadi ya mikoa ambayo itashiriki katika zoezi hilo.
 Mbunge wa Longido Mh.Michael Lekule Laizer akiteremka ndani ya pikipiki maalum ya kubebea wagonjwa aliyopewa na Waziri mkuuMizengo Pinda kusaidia wananchi wa jimbo lake leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hadji Mponda (katikati) akizungumza na Bw. Anic Kashasha (wa pili kutoka kushoto) mtendaji mkuu wa kampuni ya Tricy Solutions ya jijini Dar es salaam inayojihusisha na utoaji wa huduma  na biashara ya  vifaa vya umwagiliaji wa dawa za kuulia wadudu, Bajaj au Pikipiki maalum za kubebea wagonjwa na vifaa vya kuzimia moto leo katika viwanja vya Bunge Dodoma.
Raia wa kigeni wakitoka ndani ya ukumbi wa bunge leo  mjini Dodoma ambako walipata fursa ya kufuatilia mijadala ya wabunge.Picha na Aaron Msigwa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages