Wasanii wa Kikundi cha Sanaa na Burudani cha Gifted Yourth Tanzania, (GYT) lenye maskani yake Kinondoni Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao wa kusakata dansi wakati walipofika Kituo cha Daladala cha Mnazi Mmoja leo mchana na kuanza kucheza dansi yaani misebene ya ukweeh, na kuwaacha hoi na mshangao kibao raia waliokuwapo eneo hilo, kutokana na wasanii hao kufanya onyesho hilo bila kuzungumza chochote na kisha kuondaka zao na kuwaacha wananchi na maswali kibao " ile ilikuwa ni nini sasa? mbona hawakutangaza chochote?
Mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha Chanel 5, Sammy Misago (kushot0) Christine Maina (mwenye Orange) na Mtangazaji wa Clouds Redio, Adam Mchomvu, wakipozi kwa picha wakati nao walipokuwa katika matembezi yao na kukuta bonge la shoo katika anga hizo nao ilibidi waweke pozi mitaa hiyo huku 'wakisugulia' jinsi vijana hao walivyokuwa wakipagawisha.
Si kina Mchomvu pekee walioganda anga hizo wakishangaa bali hata wasafiri walikuwa ndani ya daladala wakipita anga hizo pia walikuwa wakishangaa bonge la shoo.
Wasanii wa hao wakiendelea kupagawisha kwa bonge la shoo la bure.
Mtangazaji wa Chanel 5. Sammy Misago (kushoto) akikatiza katika mitaa ya Mnazi Mmoja akiwa na mchuchu, Rose Wanjiru. Baadaye waliibukia katika Shoo hilo na kuganda ga! na safari yao ikaishia mahala hapo mazeee.
Sammy na Rose wakikatiza katika Kitaa kama hivi, ambapo walikwenda kuganda katika shoo la nguvu la GYT.
Mtangazaji wa redio Clouds, Adam Mchomvu akipozi na Sheila Parruque, katika mitaa ya Mnazi mmoja leo mchana wakati wakiwa katika matembezi yao na kujikuta wakiganda katika Shoo hilo la nguvu.
Na Sufiani Mafoto
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)