GAMBA JIPYA LA CCM LAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

GAMBA JIPYA LA CCM LAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM


 Naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Viuai Ally Vuai akihutubia jana jioni. Kwa upande wake Vuai alisema kuwa kamwe wana CCM wa Zanzibar hawatoi nafasi kwa chama chochote cha upinzani kushika dola. Pia alijisifu kuwa ana mchango mkubwa katika maridhiano ya kisiasa baina ya CUF na CCM Zanzibar yaliyozaa serikali ya Mseto na umoja wa Kitafa
Katibu wa Itikad na Uenezi Nape Nnauye akihutubiana maelfu ya wanachama wa CCM jana katika viwanja vya Bakhresa. Katika hotuba yake Nape aliwaahidi wana CCM kuwa atakufa na Mafisadi  wanaotaka kukihujumu chama.
Katibu Mkuu wa CCM Wilison Mukama(Kushoto) Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Makamu Mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa wakitete jambo jana katika viwanja vya Bakhresa
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Masasi akiimba wimbo wa Pongezi kwa chama cha CCM jana. Nape alitoa burudani iliyowafurahisha sana wanachama wa CCM waliofurika katika viwanja hivyo kutokana na umahiri wake wa kuimba.
Sehemu ndogo tu ya  umati wa wana-CCM waliofurika katika viwanja vya Bakhresa jijini Dar es Salaam  jana jioni wakati wa kuipokea Sekretarieti mpya ya CCM.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages