AJALI ZA MORO POLISI LAWAMANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AJALI ZA MORO POLISI LAWAMANI

 
NA DUNSTAN SHEKIDELE,MOROGORO
BAADHI ya madereva na wananchi wameonekana kulitupia lawama jeshi la polsi mkoa wa morogoro kwa kile walichodai kwamba jeshi hilo linaonekana kutokuwa na umakini katika suala zima la udhibiti wa ajali za mara kwa mara zinazoendelea kutokea katika mkoa huu.

Madereva na wananchi hao wameyasema hayo baada ya juzi Jumapili kushuhudia kijana mmoja aliyeamua kujitolea kuongoza magari kwenye eneo la kijiji cha Sengesa Melela ambapo lori aina ya Fusso lenye namba za usajili T 277 AQQ lilianguka jirani na eneo la kwaMwarabu barabara kuu ya Morogoro-lringa na kuziba upande mmoja wa barabara hivyo kusababisha magari mengine kuhitaji muongozo wa kuvuka katika eneo hilo la ajali.

Mtandao huu ulimshuhudi kijana huyu aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Alfan Mgoli aliwa bize kuyaongoza magario yanayotoka pande zote mbili,na kwamba mwandishi wetu alishuhudia baadhi ya madereva wakimpa pesa kijana huyo kama asante kwa kuwavunja katika eneo hilo la hatari.

"Fusso hili lilianguka toka siku ya ijumaa iliyopita na mpka sasa haliondolewa wala hakuna askari yeyote aliyekuja hapa" aliserma kijana huyo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages