WAZIRI MKUU ASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA UCHUMI JIJINI DAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAZIRI MKUU ASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA UCHUMI JIJINI DAR


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wataalam wa Uchumi  jana jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa Business Roundtable 2011 uliofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski. mkutano huo maalum kwa ajili ya kuwakutanisha na serikali ili kuzungumzia maswala mbalimbali ya uchumi, nafasi za uwekezaji pamoja na matatizo yanayoikumba sekta ya biashara nchini, tatizo la mgao wa umeme nchini na athari zake kwenye uwekezaji  na namna serikali ilivyojipanga kukabiliana na changamoto hizo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijadili jambo na Balozi wa Ufaransa nchini, Jacques Champagne de Labriolle (katikati) na Balozi wa Uingereza nchini, Diane Corner (kulia) katika mkutano wa Business Roundtable 2011  uliofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam jana.
Baadhi ya wataalam wa uchumi na viongozi mbalimbali wa makampuni ya biashara  wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa mkutano maalum wa uchumi uliofanyika jana jijini Dr es Salaaam.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages