WASICHANA WOTE WALIOFAULU WACHAGULIWA KIDATO CHA TANO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WASICHANA WOTE WALIOFAULU WACHAGULIWA KIDATO CHA TANO


Waziri Wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa.
Fredy Azzah
WASICHANA wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2010 na kufaulu kwa kupata daraja la I mpaka la III (Division One mpaka Three), wamepata nafasi za kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya Serikali, huku wavulana waliopata nafasi hiyo wakiwa ni asilimia 97.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema wanafunzi wote hao wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa Aprili tatu mwaka huu kuanza masomo.
Kwa mujibu wa Dk Kawambwa, wanafunzi waliokuwa
na sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi ni 36,990 wakiwamo wasichana 11,210 na wavulana 25,780.
“Wanafunzi 36,366 ambao ni asilimia 98.31 ya waliokuwa na sifa stahili wamepangwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi, kati yao wasichana ni 11,210 sawa na asilimia 100 ya wenye sifa na wavulana ni 25,156 ambao ni asilimia 97.58 ya wanafunzi wenye sifa,” alisema Dk Kawambwa.
Wanafunzi wa kike waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi ni asilimia 30.83 ya wanafunzi wote 36,366 waliopangwa.
Mwaka 2010 wanafunzi wa kike 12,638 walichaguliwa kuendelea na masomo, ikiwa ni asilimia 42.33 ya wanafunzi wote.
Kutokana na hali hiyo, idadi ya wanafunzi wa kike waliochaguliwa kuendelea na kidato cha tano na vyuo vya ufundi mwaka huu, ni pungufu ya wanafunzi 1,428 ukilinganisha na ile ya mwaka jana.
Kwa ujumla, wanafunzi waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi mwaka jana, walikuwa 33,662. Wasichana walikuwa 12,638 na wavulana 21,024.
Kwa Habari Zaidi  <<< BOFYA HAPA >>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages