WAKAZI WA MAGOMENI KOTA WATAKA KUSAINIA MKATABA NA MANISPAA KABLA YA KUHAMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAKAZI WA MAGOMENI KOTA WATAKA KUSAINIA MKATABA NA MANISPAA KABLA YA KUHAMA

Mwenyekiti wa Wakazi wa Kota za Magomeni jijini Dar es Salaam, Nkuruma Munjoli, akizungumza na baadhi ya wakazi hao kati 644, wanaoishi katika Kota hizo wakati walipokutana na kujadili mambo mbalimbali yanayowakabili kuhusu suala la kuhamishwa katika makazi yao. Kikao hicho kilifanyika katika maeneo ya Kota Magomeni juzi. Mmoja wa wakazi hao akiomba dua kabla ya kuanza kikao hicho.














WAKAZI wapatao 644 wanaoishi Magomeni Kota jijini Dar es Salaam, juzi wameitisha kikao cha kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na agizo la kuwataka kuhama katika Kota hizo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Wakazi wa Magomeni Kota, Nkuruma Munjoli, alisema kuwa, wameamua kuitisha kikao hicho ili kuwahasa wenzao ambao tayari wamekuwa wakirubuniwa kukubali kuchukua fedha Sh 700,000 na kukabidhi mikataba yao kwa manispaa ya Kinondoni ili kuhama.

Aidha alisema kuwa baadhi yao wamekuwa wakifuatwa na baadhi ya viongozi wa Manispaa na kutolewa vitisho ambavyo huwafanya kukubali kulipwa fedha na kuhama wakati suala hilo tayari limeshaamuliwa na Mahakama Kuu kuwa haipaswi kuendelea na zoezi la kubomoa wala kuwahamisha wakazi hao hadi hapo kesi itakapokuwa imemalizika.

“Sisi wala hatujakataa kuondoka mahala hapa japo sisi si wapangaji bali ni wakazi wa maeneo haya kwani tupo hapa tangu 1951 na tumekuwa tukikaa na kulipa kodi hadi tulipozuiliwa, hivyo tunahitaji kuondoka kwa kusainiana mikataba ya kuondoka mahala hapa na kurejea baada ya kukamilika kwa hayo majengo ya kisasa ya Manispaa ya Kinondoni yanayotaka kujengwa mahala hapa,

Wenzetu wa Ilala ndivyo walifanyiwa na hadi hivi leo wapo katika majengo yao yaliyojengwa upya baada ya kuhamishwa kupisha ujenzi huo, na ndivyo tunahitaji tufanyiwe na sisi” alisema Nkuruma

Kesi ya Wakazi hao inasikilizwa katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam na inatajaria kusikilizwa tena Machi 30 mwaka huu.
Picha Na Habari Kwa Hisani Ya  SUFIANI MAFOTO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages