"MATANGAZO UBUNIFU"Hii ni Swimming Pool iliyo mbele ya mlango wa kuingilia Ofisi za Vodacom, ikiwa na picha za matangazo ya kampuni hiyo, inavutia acha mchezo.
Je Umegundua nini katika picha hizi?
Je Umegundua nini katika picha hizi?
Mtaalamu wa bidhaa wa Kampuni hiyo, Yvone Maruma (kushoto)akitoa maelekezo ya kutuma sms katika Promosheni ya kuwa milionea kila siku, ili kujishindia fedha, wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo uliyofanyika jijini Dar es Salaam leo mchana. Katikati ni Ofisa huduma na bidhaa wa Kampuni hiyo, Elihuruma Ngowi (kulia) ni Ofisa habari Matina Nkurlu.
Imeelezwa kuwa mteja wa Vodacom atatakiwa kutuma SMS kupitia simu yake ya mkononi yenye neno PESA kwenda Namba 15544, ambapo atapokea maswali na baada ya kuyajibu kwa ufasaha mshiriki atapata tiketi 20 za kushiriki Promosheni hiyo na iwapo hatajibu sahihi atapatiwa tiketi 10.
Gharama za kila ujumbe ni Sh. 550, Vodacom imeandaa jumla ya Sh. milioni 210 kwa ajili ya kushindaniwa na kila siku zitatolewa Sh milioni 3 kwa muda wa siku 70.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)