VITUKO MECHI YA TASWA NA POLISI JAMII - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

VITUKO MECHI YA TASWA NA POLISI JAMII

 
Mtangazaji wa kituo cha ITV na Redio One, ambaye ni mshambuliaji wa TASWA FC, Maulid Kitenge (kushoto), akimtoka beki wa Polisi Jamii, msanii na muongozaji wa filamu, William Mtitu.
MAOFISA wa Jeshi la Polisi nchini wakiongozwa na Kamishna Mkuu wake, Said Mwema, jana walizindua michuano ya kombe la Kamanda Kova, katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Michuano hiyo ilizinduliwa kwa mechi kati ya timu ya waandishi wa habari (TASWA FC) na Polisi Jamii ambapo TASWA walifungwa mabao 3-1.

 
Kamanda Kova akikumbatia mpira baada ya kudaka shuti la Maulid Kitenge.
 
Mshambuliaji wa Polisi Polisi Jamii, Lukas Mhuvile  almaarufu kama Joti (kushoto) wa kundi la Orijino Komedi akimtoka beki wa TASWA FC.
 
Mechi hiyo ilikuwa ikitangazwa ‘live’ uwanjani hapo na msanii wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’
 
Mchezaji wa Polisi Jamii, Jacob Steven ‘JB,’ akitoka nje ya uwanja baada ya kutolewa.
 
Msanii wa filamu, Dokii (kushoto) akitaniana na Joti (kulia) uwanjani hapo.


PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages