Mkandarasi wa Ujenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), John Malisa (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Doris Malulu (kulia) wakijadiliana jambo na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kivule, Sophia Nkokoo walipotembelea juzi kukagua ukarabati wa Jengo la wazazi unaofanywa kwa msaada wa TBL, baada ya kuharibiwa na bomu lililotokea Kambi ya Jeshi ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam, mwezi uliopita. TBL imetoa sh. mil 30 za kukarabati jengo hilo na kununua vifaa vilivyoharibiwa.
Ofisa uhusiano wa Kampuni ya bia Tanzania,Doris Malulu (kushoto) akifurahi jinsi mafundi waashi, Emmanuel Mlay na Rajab Nesto wanavyoendelea vizuri na ukarabati wa jengo la wazazi la Zahanati ya Kivule unavyoendelea, alipofanya ziara ya kukagua juzi.Jengo hilo lilnokarabatiwa kwa msaada wa TBL,liliharibiwa kwa mlipuko wa bomu lililotokea Kambi ya Jeshi ya Gongo la Mboto, Februali 16 mwaka huuPicha na Mdau Bashir Nkromo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)