KARDINALI PENGO: KUNA VIONGOZI WAMEKUA WAKITENDA MAMBO MAOVU MENGI DHIDI YA WANANCHI NA KUFICHA UOZO WAO KWA GHARAMA YOYOTE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KARDINALI PENGO: KUNA VIONGOZI WAMEKUA WAKITENDA MAMBO MAOVU MENGI DHIDI YA WANANCHI NA KUFICHA UOZO WAO KWA GHARAMA YOYOTE

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
--------------
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema viongozi ndani ya Serikali, wamekuwa wakitenda mambo mengi mabaya dhidi ya wananchi na kuficha uozo wao kwa gharama yoyote.Askofu Pengo alisema hayo jana alipokuwa anaongoza Ibada ya Misa kuwaombea watu waliopoteza maisha kwenye milipuko ya mabomu Gongo la Mboto iliyofanika eneo la Hija Pugu, jijini Dar es Salaam.

Kadnali Pengo alisema mambo yanayofanywa na viongozi hao ni pamoja na ufisadi dhidi ya mali za umma na matokeo yake ni serikali kulazimishwa kulipa mabilioni ya fedha kwa Kampuni ya Dowans wakati huduma zinazotolewa kwa wananchi ni hafifu.Alisema sakata la Dowans ni sehemu ndogo kati ya uozo mwingi unaofanywa na vigogo Serikalini na kufichwa pasipo wananchi kuufahamu.Kardinali Pengo alisema imefikia mahali baadhi ya watu wanatenda maovu na kufunga midomo watu na baadhi ya vyombo vya habari na kwamba wako tayari kutoa uhai wa watu wanaodhani ni kikwazo kwao.

Gongo la Mboto
Kadnali Pengo alizungumzia milipuko ya mabomu iliyotokea Gongo la Mboto, kuwa ni ujumbe ambao Mungu alitaka kuutoa kwa Watanzania kuwa hali siyo nzuri na hivyo ni vyema kumrudia yeye (Mungu).

“Kuna weza kusiwe na uhusiano wa moja kwa moja kati ya matukio kama haya na dhambi, lakini bado ujumbe unabaki pale pale, tusiyapuuzie. Kwani watu wa Gongo la Mboto wanadhambi kuliko watu wengine wote wanaoishi Dar es Salaam? La hasha! Tusipotubu nasi tutahangamia vivyo hivyo,” alisema Askofu Pengo Kwa Habari Zaidi
  Bofya na Endelea.....>>>>>>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages