Tafakuri Yangu Ya Leo: Ya Kakobe na TANESCO mwogopeni Mungu tujaribu kwa Mafisadi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Tafakuri Yangu Ya Leo: Ya Kakobe na TANESCO mwogopeni Mungu tujaribu kwa Mafisadi


KAMA kuna jambo linalowakera watanzania basi ni hili la Ufisadi miongoni mwa baadhi ya viongozi wetu. Watanzania wanajiuliza, iweje wao waendelee kuwa masikini ilihali wachache wanazidi kuneemeka huku wakikodi ndege kwenda kutumbuliwa vipele huko Berlin Ujerumani? Sasa mimi nina pendekezo binafsi mkiona linafaa tulifanyie kazi wadau.
Hivi mnakumbuka enzi zile za mgogoro kati ya Askofu Zakaria Kakobe na TANESCO? ,  Kakobe aliendesha harakati zisizo na umwagaji damu akazipachika jina la “TANESCO Mwogopeni Mungu !!” na fulana za njano alichapa tunazikumbuka, Sasa kwa nini na sisi tusitumie mbinu hii kuwashughulikia Mafisadi?
Na hii iwe Tafakuri yangu ya leo jamani……

Nova Kambota Mwanaharakati
“Kitendawili sio deni ukishindwa nipe mji”
0717-709618 au 0766-730256
novakambota@gmail.com
novadream.blog.com
10 Machi 2011
Njombe , Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages