SIMBA YAJIKITA KUINUA VIPAJI VYA VIJANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SIMBA YAJIKITA KUINUA VIPAJI VYA VIJANA

KLABU ya Simba imesema kwa sasa imeelekeza nguvu zake katika kuinua soka la vijana wa kuanzia umri wa miaka 14 hadi 20.

Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Simba Evodius Mtawala alisema tofauti na klabu zingine za ligi kuu, Simba ina bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuendesha mazoezi ya vijana hao kila siku.

“Kila wiki makocha huchukua fedha kwa ajili ya kuwanoa vijana wetu wa kuanzia umri wa miaka 14 hadi 20. Tuna timu tatu za vijana, ya kwanza ni ya wenye umri wa chini ya miaka 14 (U-14), ya pili ni ya U-17 na ya tatu ni ya U-20.

Zote zipo chini ya kocha mkongwe Abdallah Kibadeni akisaidiana na makocha wengine watatu akiwemo Suleimani Matola.

“Kuna vipaji vingi vya vijana ambavyo tunavivumbua kila siku na tuna uhakika tuna hazina kubwa ya wachezaji ambao wako chini ya makocha wazoefu.

“Mazoezi yetu hufanyika kila siku asubuhi kuanzia saa mbili hadi saa tano katika Uwanja wa Bora uliopo maeneo ya Kijitonyama na kuna washambuliaji warefu na wenye nguvu ambao wanajua kufunga na pia kuna mabeki na viungo hatari wenye umri wa chini ya miaka 20.

“Tutakuwa na wachezaji wazuri sana katika siku za usoni ambao watakuwa hatari na watalisaidia taifa katika kuinua mchezo wa soka nchini,” alisema Mtawala.

Akizungumzia umuhimu wa kuwa na timu za vijana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema TFF inazitaka klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara kuwa na timu imara za vijana ili taifa liwe na vipaji vingi siku zijazo.

“Sheria yetu ni kwamba, tunataka angalau kila klabu iwe na wachezaji watano wa U-20 katika kikosi chake cha kwanza. Tunajiandaa kuwa makini katika kulifuatilia suala hilo,” alisema Wambura.

STORI: EZEKIEL KITULA/GPL

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages