RAISI JK ATEMBELEA WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAISI JK ATEMBELEA WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

RAIS Jakaya Kikwete ameitaka  Wizara ya  Mawasiliano ,Sayansi na  Tekonolojia,  kuendelea  kuwekeza katika Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano(TEKNOHAMA)  kwa ajili ya maendeleo  ya nchi.

Kauli hiyo ilitolewa leo (jana) na  Rais  Kikwete wakati alipotembelea wizara hiyo, jijini Dares Salaam  kwa ajili ya  kujionea  shughuli mbalimbali.
“ Nchi hii itaendelea tukiwekeza katika TEKNOHAMA… hili nitalisisitiza kwani mafanikio yake yatapatikana  katika kipindi cha miaka 10 ijayo hadi miaka 20”,”alisema Rais Kikwete huku akiisisitiza kuwa itafute ushirikiano  kutoka mkataba wa Biligates kwene masuala ya elimu na utalii.
Rais Kikwete aliitaka wizara hiyo ijipange kwa kuwekeza katika teknolojia ya nyuklia katika suala la nishati ,  hivyo suala la  mlipuko wa  nyuklia uliotokea Japan lisiwavunje moyo bali mtazamo  wao uwe  palepale kwani umetokana na  sababu za kizamani( Old reaction).  
“Mwuanze kufikiria kwa mapana teknoloji ya nyuklia kwa ajili ya  nishati . Ni muhimu tuanze kujipanga  kwa ajili hiyo mahitaji ni makubwa na uchumi unaongezeka,” alisisitiza.
Aidha Rais Jakaya Kikwete amefurahishwa na utendaji kazi mzuri  wa wizara hiyo akitolea mfano  utekelezaji wa ujenzi wa  wa Taasisi ya Nelson Mandela kwa ajili ya mafunzo ya uzamili na uzamivu na   utafiti  wa kina kwenye maeneo maalum, yenye eneo la  ekari 3,484 katika sehemu  mbili  tofauti ambazo  ni Karangai na Tengeru.
 “Nawashukuru  sana  hamjaniangusha mnafanya kazi vizuri . Nimefurahi kuona picha ya taasisi ya Nelson, nimestaajabu sikutegemea mmefikia hatua hii,” alisema .
Awali akitoa  akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za wizara hiyo na  taasisi zake , Waziri husika,  Profesa Makame  Mbarawa alisema  eneo la Tengeru  limeshaanza kuendelezwa na taasisi inategemea kuanza shughuli zake  Julai mwaka huu.
Aliongeza kuwa  fedha za ujenzi  na ukarabati wa miundo mbinu katika eneo la Tengeru ni sh bilioni 38.7 zimepatika na kampuni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Profesa  Mbarawa  alisema udahili wa wanafunzi 100  wa uzamili na uzamivu unatarajiwa kufanywa Julai mwaka huu. Hata hivyo aliongeza kuwa taasisi hiyo itakuwa na uwezo wa udahili wa wanafunzi 15,000.  (Imeandikwa na Magreth Kinabo-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages