Mhariri wa gazeti la Mtanzania, Deodatus Balile (kulia) akizngumza na Rais wa Bendi ya Fm Academia, Nyoshi El-Saadat, wakati alipotembelea kwenye ofisi ya Kampuni ya New Habari Sinza Kijiweni Dar es Salaam, leo mchana na kumtambulisha Queen Suzy (katikati) kurejea FM.
MNENGUAJI mahiri aliyewahi kupitia katika bendi ya Fm na baadaye akaipa kisogo na kutimkia Twanga Pepeta kwa kile kilichodaiwa wivu wa mapenzi na mpenziwe G7, ambaye pia ni rapa wa Fm Academia, Suzana Godwin Chubwa ‘Queen Suzy', amerejea tena Fm Academia baada ya kushindwa kuvumilia kufanya kazi mbali na mpenziwe.
Queen Suzy aliyasema hayo wakati wa mahojiano maalum na Sufianimafoto, ambapo alisema kuwa aliamua kuhama bendi ya Fm na kujiunga na Twanga ili kubadilisha mazingira ya kazi na kujaribu kuwa mbali na mpenzi wake G7 kutokana na wivu uliokithiri baina yao.
Aidha amesema kuwa na sasa ameamua kurejea tena bendi ya Fm baada ya kugundua kuwa hakuna mabadiliko hata akiwa mbali na G7 baada ya kuwa wametengana kikazi kwa muda mrefu kidogo.
"Nimeamua kurudi Fm Academia ili kuepuka ugomvi wa mara kwa mara na mchumba wangua, rapa wa bendi ya Fm, G7, ambaye amekuwa haniamini kila niwapo kazini" alisema Suzy.
“Tumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara mimi na mchumba wangu G7, sababu kubwa ni wivu, kwani anajua ninapokuwa mbali na yeye anaweza kuzidiwa, ingawa si kweli,” alisema Queen Suzy.
“Sina tatizo na Twanga Pepeta, kwani ni bendi yangu ya zamani na nimezungumza nao nimewaaga vizuri hawana neno na mimi,” alisema Suzy.
Queen Suzy amejiunga na bendi ya Fm baada ya kureje kutoka Dubai alikokwenda kumtembelea mchumba wake G7 ambaye yuko huko kwa mkataba wa kikazi ambaye anatarajia kurudi nchini hivi karibuni.
Suzy alitambulishwa katika maonyesho mawili ya bendi hiyo, likiwamo lile la Jumamosi katika Ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho na jingine Jumapili ndani ya Msasani Club.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)