Salaam, Mkuu Josephat Lukaza
Natumai ya kuwa utakua mzima wa afya njema, mimi pia niko salama kabisa. Kwanza hongera sana kwa kazi zako za blog ikiwa ni pamoja na kutuletea habari mbali mbali za burudani , michezo na uchumi kutoka nchini kwetu na Duniani kwa ujumla Big Up Sana Mkuu na Mwenyezi Mungu akubariki uendelee mbele zaidi wewe pamoja na timu yako nzima ya matukio ya josephatlukaza. blogspot.com
Kwa niaba ya timu nzima ya Blog mpya ya Mbeya yetu, tunaomba msaada wako wa kututambulishia libeneke letu jipya la Mbeya yetu kupitia Blog yako kwa wadau wote, Tunatanguliza shukrani zetu. Asante sana na kazi njema.
JINA LA BLOG: MBEYA YETU
LINK: http://mbeyayetu.blogspot.com/
Tunapenda kuitambulisha kwa wadau wote blog yetu hii ya Mbeya Yetu, ambapo nia na malengo ni kuwaletea habari mbali mbali kutoka Jijini Mbeya, Tanzania na Duniani kwa Ujumla ikiwa unatukio la aina yeyote usisite kututumia kupitia mbeyayetu@yahoo.com . karibuni nyote na asanteni kwa kututembelea.
Kwa pamoja tunaweza.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)